Wednesday, September 02, 2015

TUNDU LISSU AZUNGUMZIA KAULI ZA DK SLAA ALIZOZITOA JANA

Akizungumza na kituo cha redio cha Sauti ya Marekani (VOA), Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Antipas Lissu amesema kuwa anashangaa sana maneno aliyoyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema Dk.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi Januari na mwezi April akathibitishwa na kamati kuu.

Akaendelea kusema ameshangaa Dk Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dk Slaa mwezi wa tano ndo alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima.

Akasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 Julai kwenye Kamati Kuu, Dk Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na Dk alilala kwenye gari.

Akasema Dk Slaa asiwadanganye Watanzania tatizo ni urais na mchumba wake na kwamba kama ameacha siasa tangu siku ya kikao cha Kamati Kuu alipoandika barua ya kujiuzulu kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu??

Kwanini anaendelea kutumia gari la chama la Katibu Mkuu na nyumba aliyonunuliwa na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote toka CHADEMA??

Sikiliza hapa chini alichosema Tundu Lissu.

Mahojiano ya Tundu Lissu na VOA Swahili
 Attached Files
Post a Comment