Wednesday, September 09, 2015

SHEREHE ZA TUZO YA KIONGOZI BORA AFRIKA MASHARIKI KWA RAIS KIKWETE IKULU

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Uganda.
Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2015 . asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu, Huduma bora za jamii na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi.
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kumbukumbu maalum ya taasisi ya East Africa Books of Records mara baada ya kupokea tuzo maalum ya kiongozi bora Afrika mashariki kwa kudumisha amani nchini na katika jumuiya ya 
Afrika Mashariki kwa ujumla hususani Kenya baada ya uchaguzu mkuu na Burundi hivi karibuni.Kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Africa Book of Records Dkt.Paul Bamutize na kulia ni Mkuu wa kitengo cha utafiti katika taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza.
4
Rais Dkt. Jakaya Mrisho akitoa hotuba yake baada ya kupokea Tuzo ya Kingozi bora Afrika Mashariki.
3
Mwakilishi kutoka ubalozi wa Uganda nchini Tanzania Bwana Stephen Kiyingi akitoa hotuba yake na ushuhuda jinsi Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika miaka kumi iliyopita.
2
Baadhi ya Wageni walihudhuria hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
7
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mabalozi kutoka nchi za Afrika ya Mashariki muda mfupi baada ya kupokea Tuzo.
6
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, mabalozi kutoka nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tassisi ya East Africa Book of Records Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
  5
Wataalamu wa Utafiti kutoka Taasisi ya East Africa Book Of Records wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada kutunikiwa Tuzo hiyo. Kutoka kjushoto ni Kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize, Watatu kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utafili cha taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza na kulia ni Afisa mwandamizi wa Taasisi hiyo Bwana Kato Issa.
(Picha zote na Freddy Maro)
Post a Comment