Monday, September 07, 2015

MWIGULU NA MWAKALEBELA IRINGA MJINI

Mwigulu Nchemba na Mwakalebela wakiwa kwenye Gari ya wazi wakielekea Uwanja wa Mwembetogwa hapa Iringa Mjini tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge.
Mwigulu Nchemba akiingia na Gari la wazi kwenye Viwanja vya Mwembetogwa hapa Iringa Mjini kwaajili ya Kumnadi Mwakalebela anayepeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kwenye nafasi ya Ubunge.
Mwigulu Nchemba ambaye yumo kwenye kikosi cha Timu ya Ushindi ya CCM,hapa akiwasili Viwanja vya Mwembetogwa kwaajili ya kuzindua Rasmi kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini kwa upande wa CCM
Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Iringa Mjini wakifuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za CCM Ubunge Jimbo la Iringa Mjini hii leo.
Ombi la Mdahalo kati ya Wagombea Urais halikupitwa kwenye mkutano huu wa kihistoria kwa Wananchi wa Iringa.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Maelfu ya Wananchi wa Iringa hii leo katika Viwanja vya Mwembetogwa wakati akifungua Kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini ambapo CCM imemsimamisha Mwakalebela.
Wananchi wakiwatayari kusikiliza sera za chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Iringa kuelekea miaka 5 ijayoya Ubunge.
Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi wa Iringa kuwa ,Taifa letu linahitaji Kiongozi Magufuli kwasababu anasifa ya Uchapakazi,Mwadilifu,Mtanzania halisi,Sio mbaguzi na hana Urafiki kwenye kazi.Hivyo watanzania wampigie Kura magufuli ifikapo October 25 Mwaka huu.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Iringa Ndg.Mwakalebela
Ndg.Mahiga ambaye ni meneja kampeni wa Mwakalebela akiwatoa hofu wananchi wa Iringa kuwa watafanya Kampeni za Amani na Utulivu na amewahakikishia wataibuka washindi mapema October 25.2015.
Mwakalebela ambaye ni Mgombea Ubunge akizugumza na Wananchi wa Iringa Mjini.Kubwa amesisitiza kuwa anazijua kero za Wananchi wa Iringa Mjini hususani maji,Miundombinu na huduma za Afya,Hivyo yupotayari kuwatumikia kwa miaka 5 ijayo kama Mbunge wao.
Wananchi wa Iringa wakishangilia mara baada ya Mwigulu Nchemba kumsimamisha Mbunge Mtarajiwa Ndg.Mwakalebela.
Hisia za Wananchi kwa chama chao,Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu Nchemba (katikati),Mbunge mtarajiwa Mwakalebela(kushoto) na Kampeni Meneja wa Mwakalebela Ndg.Mahiga(Kulia) wakiwaaga wananchi wa Iringa mjini na kuwashukuru kwa Mafuriko waliyoyaleta Uwanja wa Mwembetogwa.
Picha na Sanga Festo Jr.
Post a Comment