Saturday, September 12, 2015

KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA MH.LOWASSA MJINI SINGIDA LEO

Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, SINGIDA.
Wadau wa Singida wakitafuta namna ya kupata taswira ya Mgombea wao, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mabango yenye jumbe mbali mbali kwenye Mkutano huo.
Mkali wa Propaganda, Tambwe Hizza akisema yake kwenye Mkutano huo.

Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa mji wa Singida leo.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrance Masha akionyesha Ilani ya Chama chao kwa Maelfu ya wananchi wa mji wa Singida, waliofurika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015. 


Post a Comment