Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuimarisha diplomasia ya kimataifa kwa kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na Makamu wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, kando ya Mkutas ya Dunia ya Serikali (World Governments Summit – WGS 2026), jijini Dubai, tarehe 04 Februari, 2026.
Mazungumzo hayo yalilenga kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na UAE katika maeneo ya kimkakati ikiwemo biashara, uwekezaji, miundombinu, uvumbuzi na diplomasia ya kiuchumi, sambamba na kubadilishana uzoefu kuhusu uongozi na maendeleo ya kisasa.
Mara baada ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais Samia alipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, ishara ya heshima, urafiki na uhusiano imara unaoendelea kuimarishwa kati ya Tanzania na UAE.
Ushiriki wa Rais Samia katika WGS 2026 unaendelea kuweka Tanzania katika ramani ya majadiliano ya kimataifa, huku ukitafsiri dira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kujenga ushirikiano wa kimataifa wenye tija, unaozingatia maslahi ya taifa na maendeleo endelevu.
#RaisSamia #WGS2026 #TanzaniaNaUAE #DiplomasiaYaKiuchumi #MahusianoYaKimataifa#KaziNaUtuTunasongaMbele




No comments:
Post a Comment