Friday, September 11, 2015

UNESCO WAKABIDHI KITABU CHA MAFUNZO YA TEHAMA KWA SERIKALI NCHINI

IMG_8554

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekabidhi rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali ya China.Kitabu hicho ni matokea ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
IMG_8742
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China.

Post a Comment