Thursday, November 03, 2016

GLOBAL EDUCATION LINK YAPELEKA WANAFUNZI KATIKA VYO VYA NCHINI CHINA

Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmaliki Mollel akiwa na wafanyakazi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.
Wanafunzi wakiingia katika chumba cha ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mkurugenzi Mtendaji Global Education Link (GEL), Abdulmaliki Mollel akizungumza na wazazi waliowasindiza wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vya China.

GLOBAL Education Link (GEL) imepeleka wanafunzi 50 ikiwa ni awamu ya tatu kwa mwaka huu hiyo inatokana na uhitaji wa wataalam katika udaktari na uhandisi.

Akizungumza wakati wa safari hiyo ya wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmalik Mollel amesema nafasi ya udahili nchini ni chache hivyo kama wakala wa vyuo vya nje kuchukua nafasi kwa wanafunzi wanaokosa udahili.Amesema mwitikio wanafunzi kusoma nje ni mkubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mollel amesema kutokana na nchi kuingia katika sekta ya Viwanda wanafunzi wengi wamekwenda kusoma uhandisi wa Viwanda ili waweze kuja kuleta utaalam huo na nchi iweze kupata maendeleo

Amesema GEL inachofanya ni kuhakikisha wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje kuwa wazazi wanaweza kumudu gharama za vyuo sawa na vya ndani.Hata hivyo amesema bado wanafunzi wanasajili hivyo wazazi wenye nia ya kutimiza ndoto za watoto wawasiliane na ofisi za GEL.
Post a Comment