Friday, June 05, 2015

KINANA AWASILI SALAMA MKOANI KAGERA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Ndugu Idd Ame wakati wa mapokezi katika mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye mara baada ya kuwasili Nyakanazi mkoani Kagera ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwa amembeba  mtoto Aloyce Atukuzwe wakati wa kusalimia wananchi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma wakati wa mapokezi Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Nyakanazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake mkoani Kagera.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye akisalimia wananchi wa Nyakanazi na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakanazi waliojitokeza kumpokea ambapo anategemewa kuwa na ziara ya siku 10 mkoani Kagera.

No comments:

KIPANGULA: WAHITIMU WA HABARI WATAFAIDIKA NA MABORESHO YA KANUNI

  Na Mwandishi Wetu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amewashauri Waandishi ...