KINANA AVUNA WANACHAMA WAPYA, AMNG’OA MWENYEKITI WA (BAWACHA) CHADEMA WILAYA YA MAGU

????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa  za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi9 ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini  na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.Kinana amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia  katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MAGU-MWANZA)
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao na Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu  wakiwa tayari kupokea kadi za wananchi waliokuwa wanachama wa vyama mbalimbali wakati alipojiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kisesa wilayani Magu leo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi hizo kutoka kwa wananchi hao kushoto ni  Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo wakifungua maji kama ishara uazinduzi wa utumiaji wa maji hayo katika mji wa Magu.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchota maji mara baada ya uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipozindua kikundi cha wajasiriamali cha Magu alipokitembelea leo.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza Ndugu Anthony Diallo akisalimia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo uliofanyika kwenye ukumbi wa CCM mjini Magu
????????????????????????????????????
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano kabla ya Katibu Mkuu Kinana kusalimia wananchi mjini Magu.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Kwaya ya Magu One Thietre kikiimba wimbo maalum katika mkutano huo wa kusalimia wananchi mjini Magu.
????????????????????????????????????
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakisikiliza mkutano huo.
????????????????????????????????????
Nyumba ya Bibi Asteria Selemani inayojengwa na Mwanaye Zakaria Andrew katika kijiji cha Irungu wilayani Magu Anderw amekipatia tenda ya kufyatua matofali ya kujengea nyumba hiyo kikundi cha vijana ambacho  kimefadhiliwa mashine ya kufyatua matofali na Shirika la Nyumba Tanzania NHC.
????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza Zakaria Andrew kwa kumjengea nyumba mama yake Bi. Asteria Selemani katika kijiji cha Irungu wilayani Magu
????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kufyatua matua matofali  wakati alipokagua shughuli za kikundi hicho katika kijiji cha Irungu wilayani magu.
????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kufyatua matua matofali  wakati alipokagua shughuli za kikundi hicho katika kijiji cha Irungu wilayani magu.
????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya Bi. Asteria Selemani   katika kijiji cha Irungu wilayani magu.
????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua wa nyumba hiyo  katika kijiji cha Irungu wilayani magu akiwa ameongozana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo kushoto.

Comments