WAZIRI PROF MWANDOSYA ;MWAKA 2005 NILIKUWA WA TATU MWAKA HUU IKULU ZAMU YANGU ,ATAKA WAGOMBEA WENZAKE WASIOGOPE KUELEZWA MAOVU


Waziri asiye na  wizara maalum Prof Mark Mwandosya akiwapungia mkono
baadhi ya  wahudumu  wa uwanja wa Ndege wa Nduli Iringa wakati
akiondoka mkoani Iringa kuelekea mkoani Tabora kutafuta  wadhamini kwa
ndege  hiyo ya  kukod
Waziri Prof Mwandosya  akitafakari jambo
Dereva  wa gari  alilokodi Prof Mwandosya  Iringa na rubani  wa ndege aliyokodi waziri  huyo  wakiagana
Wadhamini wa Prof Mwandosya  wakiagana na waziri  huyo.
Waziri Prof  Mwandosya  na mkewe  akishuka katika gari la kukodi  leo  ofisi  za CCM wilaya ya  Iringa  vijijini
Waziri Prof Mwandosya  akizungumza na wanahabari mkoa
wa Iringa
Mke  wa  waziri Prof Mwandosya  ,katibu msaidizi wa CCM Iringa vijijini Bw Jackson na waziri Prof Mark Mwandosya  wakisikiliza maswali ya  wadhamini
Baadhi ya  wadhamini  wa waziri Prof Mwandosya.
Katibu  msaidizi  wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Bw Hakim Jackson (kushoto) akimkabidhi Prof Mark Mwandosya fomu yenye majina ya wadhamini  wake mkoani Iringa
Mwenyekiti  wa UWT wilaya ya  Iringa  vijijini Shakra  Kiwanga akimpongeza Prof Mwandosya
Prof Mwandosya  akiwaaga  wadhamini  wake
Prof Mwandosya na mkewe  wakiingia katika ndege tayari kwa  safari ya kwenda mkoa wa Tabora na Kigoma
 Prof Mwadosya  akifurahia kupata  fomu ya  wadhamini  wake.
…………………………………………………………………….

Na MatukiodaimaBlog WAZIRI asiye  kuwa na  wizara maalum Prof Mark Mwandosya ambae ni  mmoja kati ya  wana
chama wa chama cha mapinduzi zaidi ya 35  walijitokeza  kuchukua  fomu
za  kuomba kuteuliwa  kuwa  wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM
amesema  kuwa baada ya mwaka 2005 kushika nafasi ya tatu katika
kinyang’anyiro cha Urais ni matumaini  yake mwaka huu atafanya vizuri
zaidi kwa  kushika nafasi ya  kwanza kati ya  wote  waliojitokeza sasa.
“Wewe una  mtoto anasoma  darasa  la tatu  mfano na darasa  kati  ya  watoto
90 yeye  amekuwa  wa tatu ukiwa kama mzazi lazima utampongeza na
kumweleza  kuwa uongeza jitihada  na mtihani  ujao baada ya  kuongeza
jitihada kuwa mwanangu  nataka mtihani ujao  uwe  wa kwanza  sawa
anakujibu   sawa ……sasa  mimi mwaka 2005  nilikuwa  wa tatu sasa
unataka  kuniambia  nini tena”alihoji Prof Mwandosya  huku wote  wote
pamoja na wanahabari  wakiangua kicheko .
Akizungumza na  wanahabari  leo katika  ofisi ya  CCM wilaya ya  Iringa  vijijini
mara  baada ya  kudhaminiwa na  wanachama 28  wa CCM ,Prof Mwandosya
alisema  kuwa safari  yake ni safari ya uhakika na  hivyo iwapo  chama
chake  kitamteua kuwa  mgombea watanzania wategemee kuwa na nchi yenye
uchumi  bora .
Prof Mwandosya ambae  aliulizwa na  wanahabari hao  kuwa anajambo gani
jipya  la  kulifanya ambalo Rais anayemaliza  muda  wake Dr Jakaya
Kikwete hakufanya alisema  kuwa  si  kweli kama serikali ya Dr Kikwete
haikufanya  lolote japo alisema kiwa awamu ina changamoto  zake na kila
awamu imefanya mambo makubwa
“Kusema unalinganisha  na  serikali  iliyopo ni kama  vile  unataka  kusema
serikali  zilizotangulia hazikufanya  lolote ama hazikufikia  malengo
yaliyotarajiwa  ukweli  ni  vipindi  katika  uongozi  wa nchi  ambavyo
vinatofautiana  mfano miaka  iliyopita  mimi nikiwa  waziri  wa
mawasiliano na  uchukuzi simu  hizi  za  mikononi ambazo matumizi yake
ni makubwa hazikuwepo ila  sasa  kuna  simu ambayo ni kamera ,Voice
recoda na pia  ni kopyuta  hiyo  hiyo  sasa huwezi  linganisha  miaka
hiyo na  sasa na huwezi  sema serikali iliyopita haikufanya ukweli
kila  serikali imefanya kulingana na  wakati wake.”
Alisema kuwa atafanya zaidi ya serikali  iliyopita ama  chini ya  serikali
iliyopita bado  si  jibu la kumsaidia mtanzania kwani  alisema  katika
ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 -2010 ujenzi  wa  chuo  kikuu  cha
Dodoma haukuwepo na wala haikuwa ni ahadi ya Rais Dr  Kikwete  ila
kutokana na kuna kuna haja ya  kuanzisha  chuo  hicho serikali  iliweza
kuadhimia na  kufanikiwa  kuanzisha  chuo  hicho ambacho ndicho  chuo
bora nchini na Afrika Mashariki .
Hata  hivyo  alisema  kuwa kwa  kuwa kipaumbele  chake  kikubwa ni  kujenga
uchumi bora  pia ana amini kupitia uchumi bora  hakuna jambo
litakaloshindikana kwani katika uchumi bora itakuwa ni  vigumu
kuzungumzia  uchumi  bora kama miundo  mbinu haitaboreshwa  wala bila
kuwepo kwa  kilimo na masoko  ama  kuwa na masoko  bila  viwanda au
kuzungumzia kukuza  uchumi bila  kuwa  na elimu  bora .
Prof  Mwandosya alisema  kuwa mbali ya  kuwa ni  waziri ila bado anaishi na
jamii na pia anatambua mazuri  mengi  yaliyofanywa na Rais Dr  Kikwete
na  changamoto  zake   hivyo akiingia  Ikulu lazima yale mazuri  yote
yaliyofanywa na serikali  iliyopita atayaendeleza  zaidi  ya hapo
yalipoachiwa na zile  changamoto  kuweza  kuzitafutia majibu  sahihi kwa
faida ya  jamii ya  kitanzania.
Pia alisema mambo  mengi anayatambua vema kwa  kuwa  yupo  jikoni na
mengine anayatambua vizuri  kutoka kwa jamii ambayo imemlalamikia  hivyo
jukumu la kuyatekeleza lipo  mikononi mwake na kuwataka  wananchi hasa
wana CCM kuendelea kujenga  imani zaidi kwake .
“Lazima  kuwa na vipaumbele ambavyo  ni majibu ya mwananchi katika
kukuza  uchumi kwani  huwezi chukua elimu ukaacha  miundo  mbinu kwani
miundo  mbinu ndio  itakuza uchumi na  huwezi  zungumzia afya  bila
kuboresha elimu ….ukifanya haya makubwa manne hapo ndipo unageukia
upande  wa pili…..niseme  tu kuwa uchumi unapokuwa lazima
unazungumzia takwimu na  kuona kipato  cha Taifa  kinaongezeka”
Waziri Prof Mwandosya  alisema kuwa katika utawala  wake kama Rais ni  kuona
anakuza  uchumi  zaidi kupitia  kilimo huku akiamini  kuwa  asilimia
zaidi ya 80 ya watanzania  wanategemea  zaidi  kilimo katika  kuendesha
maisha  yao na  kilimo pia kinaweza  kukuza  uchumi  haraka  zaidi .
Katika hatua nyingine Prof Mwandosya amewataka  wagombea wenzake kuheshimu
taratibu  za CCM katika mchakato  wa  kutafuta  wadhamini badala ya
kugeuza mbio hizo kama   sehemu ya kuonyesha umarufu usio na  tija na
kuwa utaratibu  wa  CCM ni  kupata  wadhamini 450 pekee  pasipo
mbwembwe  za aina  yoyote pia vigezo  vya mgombea  wa  urais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania vipo wazi  kuanzia kiwango  chake  cha elimu na
awe na miaka kuanzia 40  kuwataka   wote watia nia  kujitathimini badala
ya  kuingiza mchezo katika  suala  hilo nyeti.
Prof Mwandosya aliwataka  wagombea wenzake  ndani ya CCM wasilalamike kwa
kukumbushwa ukweli na madudu waliyoyafanya wakati  wakiwa  serikalini
kwani ni  vigumu watanzania  kusahau maovu ya mgombea yeyote na  kuwa
anachojivunia yeye katika uongozi  wake toka kipindi  cha hayati baba wa
Taifa  hadi  sasa hajapata  kuwa na sifa mbaya kama baadhi ya
wagombea  wengine ambao  wamechukua fomu ya  kuomba kuaminiwa na CCM
mbali ya kuwa na sifa mbaya kwa Taifa .
Pia alieleza  kusikitishwa na matumizi makubwa ya pesa katika mchakato  huu
na kuwa anashangazwa kuona wana CCM wakiendelea kuchezea pesa kwa
kuandaa mbwembwe nyingi mikoani kwa ajili ya mapokezi yao wakati kila
mgombea alipewa taratibu na chama juu ya nini afanye wakati  wa
kuzunguka kutafuta  wadhamini na  kuwa pesa  zinazotumia zingeweza
kusaidia miradi ya  kijamii kuliko kuzimwaga kama njugu kwani ni hatari
kwa uhai  wa chama .

Comments