Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuaindua rasmi kivuko cha Super Sumar kinachofanya safari zake kati ya Pwani ya Kamanga wilayani Sengerema na Mwanza wakati Katibu Mkuu huyo alipo fanya ziara katika jimbo la Sengerema leo akikagua, Kuhimiza na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi. Huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katika picha kutoka kulia ni Miraji Mtaturu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. William Ngeleja, kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanzan Ndugu Magesa Mulongo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine ya Mwanza Salum Ali wakishiriki katika uzinduai huo uliofanyika katika Feri ya Kamanga wilayani Sengerema.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SENGEREMA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kivuko cha Super Sumar akiwa ameongozana na viongozi wa mkoa wa Mwanza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chumba cha kapteni wa kivuko hicho mara baada ya kukizindua rasmi katika feri ya Kamanga wilayani Sengerema.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha kivuko hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Sengerema Mh. William Neleja, katikati ni Kada wa CCM Bw. Laurence Masha na kulia ni Mkurungenzi wa Songoro Marine ya Mwanza Bw. Salim Ali.
Mbunge wa Sengerema Mh. William Neleja akizungumza katika uzinduzi huo huku Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akimsikiliza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amesema ni muhimu kuitengeneza barabara ya Kamanga Sengerema kwa kiwango cha lami ili kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi wanaotumia feri hiyo ya Kamanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria katika kijiji cha Nyamazugo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anhony Sanga Mkurugenzi wa MWAUWASA wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji wa Sengerema na vijiji vyake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilagua mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji wa Sengerema na vijiji vyake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anhony Sanga Mkurugenzi wa MWAUWASA wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la maji katika eneo la Igogo mjini Sengerema ambalo litapokea maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji wa Sengerema na vijiji vyake.
Hii ni sehemu ya tanki la maji linalojengwa katika keneo la Igogo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mhandisi Anhony Sanga Mkurugenzi wa MWAUWASA wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la kupokea maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji wa Sengerema na vijiji vyake, Katikati ni Mbunge wa jimbo al Sengerema Mh William Ngeleja na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu mwenye kofia.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi huo kutoka kushoto ni Miraji Mtaturu Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza , Mhandisi Anhony Sanga Mkurugenzi wa MWAUWASA na Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. William Ngeleja wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la kupokea maji linalojengwa eneo la Igogo kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji wa Sengerema na vijiji vyake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na ukaguzi huo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anhony Sanga Mkurugenzi wa MWAUWASA wakati alipokagua mradi huo.
Mafundi wakiendelea na kazi katika mradi huo
Miraji Mtaturu Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza akizungumza na wananchi wakati akimkaribisha Ndugu William Ngelea kupanda jukwaani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM mjini Sengerema.
Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. William Ngereja akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Sengerema.
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Sengerema.
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Sengerema.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM mjini Sengerema
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu matatizo ya wananchi katika mkutano huo.
Umati wa wananchi akiwa umefurika katika mji wa Sengerema.
Comments