ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA KWIMBA MKOANI MWANZA

Sehemu ya Umati wa wakazi wa wilaya ya Kwimba na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara,Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya jana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, Ndugu Kinana alikemea tabia ya wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza kuwatekelezea kila kitu,aidha aliwataka vijana wa kitanzania kuacha kabisa kuhadaika na baadhi ya Wanasiasa ambao wamekuwa wakiwapotosha na kuamini kila kitu kitapatikana bila kufanya kazi na kujituma.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
Wananchi wilaya ya Kwimba wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya jana.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Mh., Shanif Mansoor akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya jana. 
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHADEMA katika Kijiji cha Ilula kata ya Ilula wilayani Kwimba,ndugu AmaraMateremki  akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akionesha baadhi ya kadi za wafuasi wa chama cha CHADEMA kuhamia CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor pichani shoto.
Mmoja wa viongozi kutoka kikundi cha akina mama kiitwacha UAMSHO akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mara baada ya kukabidhiwa vyerehani vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor .
 Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiongea kwa balozi wa shina namba 12,Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.

Comments