ZIARA YA KATIBU WA CCM NDUGU KINANA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani Mbongwe,mkoani Geita.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwaga zege katika zahanati ya kijiji cha Kasheko kata ya Lulembera wilayani Mbogwe mkoani Geita. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa wodi ya akina mama inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Lugunga
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipaka rangi moja ya nyumba za walimu zinazojengwa kwa nguvu za wananchi katika sekondari ya Mbogwe kata ya Bwela.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lugunga,wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na Wana CCM katika katika kata ya Mang'ombe kwenye kikao cha Halmashauri kuu Wilaya pamoja na kupokea taarifa ya chama na serikali
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe,Dkt John Mgosha,alipokagua kituo hicho na kuwasha umeme wa REA kituoni hapo,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.Kinana na ujumbe wake yupo katika ziara ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010-2015 inayotekelezwa na serikali. 
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na kazi zinazofanywa na vikundi vya wajasiliamali-Wanawake mjini Masumbwe wilayani Mbogwe,Ndugu Kinana alikagua miradi mbalimbali ya vikundi hivyo vya wajasiliamali.
 Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa Masumbwe,wilayani Mbogwe mkoani Geita.
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe.

PICHA NA MICHUZI JR-MBOGWE, GEITA

Comments