Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka jiwe la msingi katika nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi ambazo ujenzi wake utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimia viongozi wa NHC mara baada ya kuwasili eneo la Napupa Masasi kuzindua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC. Anayemuongoza Mh. Waziri ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na hadhira iliyofurika katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.Alizitaka taasisi zinazotoa huduma ya umeme na maji kutekeleza majukumu yao ili kupunguza gharama za uuzaji wa nyumba zinazojengwa na waendelezaji wote wa makazi.
Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi. Akitoa taarifa ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi kwa Waziri wa ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi aliyefika katika mradi huo wenye nyumba 54 na kuuzindua.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Bi Beatrice Dominic akitoa taarifa ya usimamizi wa ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi alipozuru Masasi na kuzindua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na wazee aliyowahi kufanya nao kazi Wilayani Masasi mwaka 1975 akiwa Katibu wa Vijana wa Wilaya, baada ya kukutana nao Ikulu ndogo Mjini Masasi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi,akionyeshwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Bi. Bi Beatrice Dominic mali na magari yaliyounguzwa na vijana wa Masasi kutokana na vurugu zilizowahi kutokea huko nyuma na kuunguza pia jengo la Ofisi ya ardhi ikiwemo nyaraka zote. Hadi sasa Halmashauri hiyo haina Ofisi za kutosha kufanyia kazi na wala usafiri wa kusaidia utendaji wa kazi wenye tija.
Comments