WANAKIJIJI ITUNDU KATA YA MLANGALI WATAKA FILIKUNJOMBE KUENDELEA UBUNGE WAMCHANGIA TSH 65,200 ZA FOMU
Wananchi wakimchangia mbunge Filikunjombe pesa za kuchukua fomu ya ubunge |
Mbunge Filikunjombe akichangiwa pesa ya kuchukulia fomu ya ubunge muda ukifika |
Mbunge Filikunjombe akifurahia kuchangia pesa ya kuchukulia fomu ya ubunge |
Wananchi wa kada mbali mbali wakimchangia mbunge Filikunjombe |
Filikunjombe akikabidhi sare kwa madereva boda boda Mlangali |
Kwaya ya vijana wakiimba wimbo wa kulinda amani wakati wa mkutano wa mbunge Filikunjombe. |
Mbunge Filikunjombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itundu kata ya Mlangali Ludewa. |
Filikunjombe akitoa mfano wa mshikamano wa kimaendeleo unavyoweza kuleta mabadiliko makubwa. |
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu zote 8 za vitongoji vya kijiji cha Itundu kata ya Mlangali |
Na matukiodaimaBlog,Ludewa
WANACHAMA waasasi za
fedha vijijini kutoka vikundi zaidi ya saba vya Vicoba na
Sliki pamoja na wananchi wa kijiji
cha Itundu kata ya Mlangali wilaya
ya Kilolo mkoani Njombe wamemchangia
mbunge wa jimbo la Ludewa
Bw Deo Filikunjombe kiasi cha Tsh
65,200 kwa ajili ya kuchangia fedha za
kuchukua fomu ya kuwania ubunge kwa muhula wa pili katika
jimbo hilo la Ludewa.
Pamoja na kuchangia pesa hiyo
pia wakazi wa kata hiyo
kupitia wazee wa kijiji
cha Itundu walikitaka
chama cha Mapinduzi (CCM) kutoruhusu wana CCM
wengine kuchukua fomu ya ubunge
katika jimbo la Ludewa ili wao kuweza
kuendelea na mbunge wao
wa sasa kutokana na
utendaji kazi wake kiasi cha kuwakomboa
wananchi wa Ludewa .
Wananchi hao waliyasema
hayo jana kwa nyakati
tofauti wakati wa hafla
ya uziduzi wa vikundi hivyo na
mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja wa Stendi katika kijiji
hicho cha Itundu .
Mzee Augustino
Msemakweli na mzee Herbert Kayombo walisema
kuwa ni mbunge
wa kwanza kwa jimbo hilo la Ludewa
kati ya wabunge zaidi ya 6
waliopata kuongoza kufanikisha utekelezaji
wa ahadi zake kwa wakati na kuwa wao kama
wazee wa kijiji hicho na ni miongoni mwa wazee wa jimbo la Ludewa ambao ni makada wa
CCM kilio chao kwa sasa ni kuona mbunge huyo anaendelea kuongoza jimbo hilo zaidi
pamoja na kuwasaidia kuwapigania
wazee ili kuweza kuliptwa mafao ya uzeeni kutoka serikalini.
Mzee Msemakweli alisema
kuwa amepata kusoma moja kati ya gazeti la wiki kutoka Zanzibar na
kuonyesha ni kiasi gani serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ilivyoweka mkakati wa
kuwasaidia wazee kwa
kupanga kumlipa mafao mzee kila mwezi
kiasi cha kuanzia Tsh 20,000 hivyo
kuomba mbunge wao kuendelea kuungana
na wabunge wengine ili nao
waweze kulipwa mafao ya uzeeni.
Wakati mzee
Kayombo akieleza kufurahishwa na
utendaji wa Filikunjombe na kusikitishwa
na mbinu chafu za upinzani katika
kata hiyo inayoongozwa na diwani wa chadema na mwenyekiti wa Chadema kuwazuia wananchi kulima katika
mabonde ( Vinyungu)na kuwa wanafanya
hivyo kwa lengo la
kukwamisha jitihada za mbunge
wao.
Kwani alisema katika
kijiji hicho wananchi miaka yote
walikuwa wakilima kwenye vinyungu
kutokana na eneo hilo kutokuwa na chanzo cha maji na
hata umeme wanaotegemea
kupata hauzalishwi katika kijiji
hicho .
Alisema kuwa serikali
ya kijiji inawataka
wananchi kutolima umbali wa mita 60 ya
mto wakati umbali huo ni mkubwa
ukilinganisha na ukubwa wa
eneo hilo.
Kuhusu mtazamo
wa wananchi wa
Ludewa juu ya utendaji kazi wa mbunge
huyo alisema wao kama wazee wamefurahishwa na kazi zinazofanywa na mbunge huyo na
kuwa wao kama wapiga kura
wanahitaji mtu na sio chama na kama chama kitaona Filikunjombe
hawafai wao kama wananchi hawatakuwa tayari kuunga mkono
maamuzi yoyote nje ya matakwa yao.
Hata hivyo alisema
kuwa changamoto kubwa ya kijiji
chao kwa sasa ni maji na umeme na kumshukuru mbunge kwa kuwasaidia
gari la wagonjwa katika kijiji na kata yao ya Mlangali .
Kwa upande wake Emmanuel
Mpogole akizungumza kwa niaba ya wanachama
wa vikundi vya kifedha vijijini alisema kuwa kumekuwepo na hamasa kubwa ya uanzishwaji wa
vikundi hivyo toka alipoingia mbunge huyo madarakani na kuwa hali ya uchumi wao
imezidi kuboresheka zaidi.
Akizungumza na
wananchi hao mbali ya kuwashukuru kwa mchango wao wa fedha za
kuchukulia fomu Bw Filikunjombe
alisema kuwa imani ambayo wananchi
wanaionyesha kwake ni kubwa na
kuwa mbali ya kutumia kiasi cha Tsh milioni 75 kwa wilaya nzima kila mwaka kusomesha
watoto zaidi ya 20 kila kata bado kata
hiyo ya Mlangali ndio kata pekee ambayo
mmoja kati ya wanafunzi
aliowasomesha alifika kushukuru na hivyo kwa mwaka mwakani kata
hiyo atasomesha watoto 30 badala
ya 25 kama kata nyingine.
Pia alisema suala la
maji bado wa kulaumiwa ni viongozi wao wa kijiji ambao hata katika taarifa ya kijiji
kwa mbunge hawaonyeshi kama wana tatizo
la maji kama viongozi wa vijijini vingine ambao taarifa zao
hueleza wazi changamoto mbali
mbali .
Bw Filikunjombe alisema mbali ya viongozi wao kutoeleza
tatizo hilo la maji ila kwa upande wake analichukua ili
kuanza kushughulikia kumaliza
kero ya maji katika kijiji hicho .
Mbunge huyo
katika kuunga mkono vikundi vya
kifedha vijijini aliahidi kusaidia
kutoa mafunzo ya ujasliamali
kwa wanachama wote
wa vikundi zaidi ya 7 vya kifedha
vijijini pamoja na kila kikundi kukichangia kiasi cha Tsh 500,000
huku kikundi cha boda boda akikichangia kiasi cha Tsh
milioni 2.
Comments