WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU, ALAKIWA NA WAFUASI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA NYAMAGANA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akipokewa na wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ofisi za Chama hicho wilaya ya Nyamagana, wakati alipofika kusaka wadhamini jijini Mwanza. Mamia ya watu walijitokeza kumdhamini.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akionyesha fomu baada ya wanachama wa CCM kumdhamini, ambapo alidhaminiwa na wanachama.
MAMIA ya wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkumbi wa mikutano wa CCM Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipokwenda kuomba udhamini kuomba kuteuliwa kuwa mgombea urais wa CCM.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiagana na wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini mjini Bariadi mkoani Simiyu, juzi, wakati alipokwenda kuomba udhamini.
Comments