KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF), MWESIGWA SELESTINE ATAMBUISHA KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS

mail.google.comKocha Mkwasa (kushoto),na Msaidizi wake Hemed Morocco wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.
Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.
Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.
Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Comments