Monday, June 22, 2015

KAIMU MKURUGENZI BOHARI YA DAWA (MSD), AZUNGUMZIA UFUNGUAJI MADUKA YAO KARIBU NA WANANCHI

 

 Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), akimuelekeza jambo Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kushoto), akizungumza na John Chale kuhusu kazi mbalimbali zinazpfanywa na MSD baada ya kutembelea banda la MSD katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki
 Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kushoto), akiwaelekeza jambo wananchi waliotembelea banda la MSD katika maonyesho hayo.
 Vifaa tiba mbalimbali na vitanda vinavyoonyeshwa na MSD katika maonyesho hayo.
Kitanda kikiwa kwenye soko kwenye maonyesho hayo.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI Kuu ya Dawa (MSD),imejipanga  kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufungua maduka yao kwenye mikoa minne nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani katika mahojiano ya maonyesho ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mwaifwani alisesema lengo ni kuziondolewa usumbufu hospitali kuagiza dawa kwenye ofisi ya kanda mara zinawaishia ghafla na maduka hayo yatakuwa ndani ya hospitali au karibia na hospitali.

Ametaja mikoa ambayo wanaanzia kufungua maduka hayo  ni Mbeya,Dar es Salaam,Mwanza na Arusha ambamo yatakuwa yanafanyakazi saa 24.

“Tumeamua kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua maduka katika mikoa hiyo aidha,ndani ya hospitali au karibu na hospitali kuzirahisishia kuzinunua pindi wanaishiwa na dawa kabla ya kuziagiza”,alisema Mwaifwani .

Akizungumzia mafanikio alisema wamepata  muarobaini ya kuwadhibiti wezi wa dawa za serikali kwa kuziwekea nembo maalum.

Alisema tayari  zoezi hilo lishaanza ambapo hadi sasa dawa 42 zishawekewa nembo hizo zijulikanazo kama (GOT), na jitihada bado zinaendelea kwa dawa nyingine.

Mwaifwani alisema  jitihada bado zinaendelea kufanywa na MSD kuendelea kuziweka nembo zaidi dawa nyingine za kawaida ambayo jumla yake ni 630,na zile za mradi msonge jumla yake 613.

“MSD bado inaendelea kuweka dawa za serikali nembo ili kudhibiti wizi wizi na tumeanza na aina hizo 42 bado tunaendelea kuweka nyingine zilizobakia”,amesema Mwaifwani.

Amezitaja baadhi ya dawa zilizowekewa nembo kuwa ni pamoja na Magnesium, Amoxilin, Ciproflaxin, paracetamol, Dixlophenac,  Clotromoxin na nyinginezo.  (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: