HUAWEI TANZANIA NA WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA NCHINI

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na kampuni ya Huawei katika kongamano la Teknohama, kulia ni Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala.
Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kongamano la Teknohama kushoto ni Mkurugenzi wa ICT katika wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba (Kushoto) wakishikana mkono na Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kuashilia kuungana katika kongamano la Teknohama.

Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Technolojia jana ilitangaza kuwepo kwa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Center JNICC tarehe 18 na 19 Juni 2015.

Kongamano hilo litajadili hali ya sekta ya tecknohama kwa sasa,sera mpya zitakazowekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini.pia kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake ya milenia kupitia tecknohama.

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Dk. Ally Simba alisema, “tumefurahi sana kwamba Wizara na kampuni ya Huawei Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo,ambapo tutajadiliana kwa undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT.Na kwa upande wa Wizara tutaelezea sera mpya na mipango tulioweka ili kuhakikisha maendeleo ya sekta”.

Aliendelea kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba Wizara imejikita katika kukuza sekta ya Teknohama.aliongeza kwamba Makamo wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi,huku pia ,Waziri na Katibu Mkuu wa Wizaraya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Balozi wa China nchini Tanzania watakuwepo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala alisema, “tunaishukuru sana Wizara kwa kukubali kuungana nasi katika kuandaa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference nchini Tanzania,na tunawahakikishia Watanzania wote kwamba kongamano litapendeza.

Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.

Katika kongamano hilo,Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na Fusonq.Pia kutakua na gari maalumu la kufanya maonesho,gari hilo kwa kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani,na kwa mwaka wa 2015 litazuru bara la Afrika haswa Afrika kusini na Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo ya nchi itakayopita.

Comments