KINANA AKUTANA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ILYANCHELE WILAYANI BUKOMBE

????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukivuka mto kuelekea katika kijiji cha Ilyanchele wilayani Bukombe wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika wilaya hiyo kuelekea katika kijiji hicho hata hivyo msafara huo haukuweza kuvuka mto mkubwa wa Ilyanchele na magari  kutokana na kutokuwepo kwa daraja linalounganisha kijiji hicho ambapo leo ndiyo limewekwa  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo  na Ndugu Abdulrahman Kinana.
Baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo Kinana pamoja na msafara wake walivuka mto huo kwenye daraja la miti lililotengenezwa kwa nguvu za wananchi.  kisha alipanda pikipiki na kuelekea katika mkutano mdogo na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele ambacho kimo katika msitu wa akiba  kata ya Nyamonge wilayani Bukombe mkoani Geita.
Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza ambapo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Kagera sasa anaendelea na ziara hiyo katika mkoa wa Geita kabla ya kumalizia ziara yake mkoani Mwanza akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUKOMBE-GEITA)
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja la mto Ilyanchele wilayani Bukombe.
????????????????????????????????????
Maandalizi yakiendelea tayari kwa ajili ya ujenzi huo.
????????????????????????????????????
Hili ndilo daraja la miti linalotumika kwa sasa huku mifugo pia ikivuka katika mto huo
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka pamoja na wananchi katika daraja hilo lililotengenezwa kwa miti.
????????????????????????????????????
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akivuka na wananchi katika daraja hilo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakivuka katika daraja hilo.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepanda pikipiki akielekea katika kijiji cha Ilyanchele kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakimpungia mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati wa mkutano huo.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hao katika mkutano mdogo uliofanyika kijijini hapo.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye anayepiga ngoma wakisindikizwa na kikundi cha ngoma pamoja na wananchi mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka tena mto huo wakati akirejea upande wa pili ili kuendelea na ziara yake.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akila muwa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Bukombe wakati akirejea mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele.
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana wachimbaji wadogowadogo wa madini wa kata ya Uyovu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kilirudisha mikononi mwa CCM jimbo la Bukombe 
????????????????????????????????????
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Runzewe.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Runzewe
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kazi ya kutega mizinga ya nyuki kwenye mradi wa ufugaji nyuki wa katika shule ya sekondari ya Busonge kata ya Iyogelo
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Ushirombo wilayani Bukombe.
????????????????????????????????????
Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Ushirombo
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Ushirombo.
????????????????????????????????????
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano huo.

Comments