Wednesday, June 17, 2015

WATANZANIA WANATAPELIWA SARAFU HII YA SH. 500 HAINA THAMANI YOYOTE NI UZUSHI-MENEJA UHUSIANO WA BENKI YA TANZANIA BOT, ZALIA MBEO

index
Na Salma Ngwilizi – Maelezo
………………………………
 Benki  ya Tanzania(BOT) imewataadharisha wananchi kwamba  sarafu  ya sh. 500 haina  madini ya aina yoyote  na wala  haiuzwi  kama inadaiwa baadhi ya watu.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja  Uhusiano wa benki hiyo,  Zalia Mbeo wakati akitoa ufafanuzi kwa  Kaimu  Katibu Mkuu wa  Ofisi ya Rais Menejimenti ya  Utumishi wa Umma, HAB  Mwizu  ambaye aliuliza kwamba  kuna taarifa  kuhusu sarafu  hiyo kuuzwa mitaani .
 Kaimu Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  Mhe. Celina Kombani.
 “Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.
 Aliongeza wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini ambayo  yanaweza kuwapatia fedha nyingi  wakati si kweli.
 Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa rasmi   leo Juni 16, mwaka huu na yanatarajia kumalizika Juni 23, mwaka huu.
 Kauli mbiu ya mwaka huu “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake  kuongeza Ubunifu  na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.

No comments: