Wednesday, June 24, 2015

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.CHAFANA

5
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi akizungumza na watumishi wa Umma na wananchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ,Juni 23,2015.
2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akihutubia wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
3
Moja kati ya washindi wa tuzo za Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 wakifurahia tuzo waliyoipata wakati wa kilele za Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
4
Baadhi ya Watumishi wa Umma na wananchi waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani)
6
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akimkabidhi tuzo mmoja wa wawakilishi wa taasisi zilizopata tuzo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
7
Tuzo zilizokabidhiwa Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
1
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi  (wa pili kutoka kushoto) akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana. Anayemuongoza ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (watatu kutoka kushoto.

No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...