Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akisoma hotuba yake wakati akifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam-Juni 16,2015.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu(kushoto) wakati akipata maelezo katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam (Kulia ), Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bi Rose Mdami.
…………………………………………………..
Na Salma Ngiwilizi – Maelezo
Serikali imewataka watumishi wa umma nchini kuonyesha ubunifu na weledi katika utendaji kazi wa majukumu yao mbalimbali ili kuweza kukidhi matarajio ya wananchi .
Aidha imewasisitiza watumishi wa umma wanawake kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ufanisi ili kuonyesha uwezo wao na uhodari katika kutekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wakati akifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja .
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.
Serikali imetoa miongozo mbalimbali ya kisera inayokusudia kumpa mwanamke wa nchi hii fursa sawa ya kuchangia maendeleo ya nchi yetu . Baadhi ya miongozo hiyo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, na mwongozo wa anuai za jamii mwaka 2010.
Alisema hadi sasa utekelezaji wa miongozo hii umeleta matokeo chanya ambapo nchi yetu inajivunia kufikia mafanikio kadhaa , ambayo ni pamoja kuongezeka kwa idadi hya wanawake katika ngazi za maamuzi Serikalini kutoka asilimia 26 mwaka 2005 na kufikia asilimia 34 mwaka 2014.
“Wale waliopata nafasi walizopewa au kupata kutokana na juhudi zao. Ujuzi au uzoefu wao wanazitendea haki kwa kusimamia vizuri wale walio chini yao na kutoa huduma bora iliyotukuka kwa wananchi,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa mafanikio mengine ni kujenga uwezo wa watumishi wanawake kupata sifa za ziada ,kuongeza ubunifu na kuboresha upatikanaji wa huduma na Serikali imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili kwa wanawake katika Vyuo Vikuu vya hapa nchini. Hivyo katika kipindi cha miaka 10 jumla ya watumishi wanawake 251 walipatiwa ufadhili na kuhitimu masomo yao katika shahada mbalimbali za uzamili.
Alitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,sekta binfasi na vyombo vya habari kuendelea kutoa mchnago katika kuhimarisha Utumishi wa Umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Comments