Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Zhang Yongquan akitoa hotuba yake katika kongamano la Huawei Cloud Conference 2015, wakitazama (kutoka kushoto hadi kulia); Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lv Youqing.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu na Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Zhang Yongquan wakitia saini Mkataba wa Makubaliano (MoU), kati ya Huawei Tanzania na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambapo Huawei watakuwa washauri wakuu wa nchi katika maswala ya TEHAMA. Wakitizama (kutoka kulia hadi kushoto); Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lv Youqing na Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Kombo.
Kushoto hadi kulia; Mkurugenzi wa TEHAMA katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dr. Ally Simba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngodo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Kombo, Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lv Youqing na Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Zhang Yongquan wakijitayarisha kuzindua bidhaa mpya za teknolojia za Huawei; OceanStor V3 na FusionCube katika kongamano la Huawei Cloud Conference 2015.
Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Zhang Yongquan na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa wakikata utepe kuzindua rasmi gari maalum la Huawei kwa ajili ya maonyesho.
…………………………
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Prof. Makame Mbarawa ameipongeza HUAWEI Tanzania kwa ushirikiano wao wa karibu na wizara katika kuchangia miradi mingi hususan mambo mengi ya TEHAMA .
Huawei Tanzania inafanya kazi kwa ukaribu sana ni wizara na kwa hivi sasa ni mojawapo ya supplier wa vifaa vingi vya ujenzi wa jingo jipya la DATA center.
Data center ni mojawapo ya ujenzi mkubwa unaofanywa na wizara ya sayansi na jingo hili litakua na kazi ya kuhifadhi DATA za serikali pamoja na makampuni mbalimbali ya umma na ya binafsi. Data center itakuwa inahifadhi na kutunza kwa usalama takwimu na habari zozote kwa kutumia sever zake na kupelekea upatikanaji wa huduma kua kwa bei nafuu na kwa urahisi

Comments