Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiswaga Ng’ombe ili kunywesha kwenye Lambo la kisasa la kunywesha mifugo la kijiji cha Mwagi Kishiri katika jimbo la Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kinana amemaliza ziara katika jimbo hilo na kesho anaendelea na ziara katika jimbo la Magu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SUMVE-KWIMBA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana shea mifugo kushoto na Mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa wakiangalia Lambo la Kisasa la kunyweshea mifugo lililojengwa katika kijiji cha Mwagi Kishiri jimbo la Sumve wilayani Kwimba
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na kumpongeza mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa kushoto na Halmashauri ya wilaya ya Kwimba kwa kujenga Lambo hilo na visima vya maji kwa ajili ya wananchi wa vijiji hivyo, kutoka kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu na Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bi. Pili Moshi.
mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa akitoa maelezo yake mbele ya Kinana kuuelezea mradi huo wa maji kwa ajili ya mifugo na binadamu.
Mifugo ikinywa maji l katika lambo hilo la kisasa katika kijiji cha Mwagi Kishiri Sumve wilayani Kwimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea chanzo cha maji kilichopo Mwagi Mwabilanda.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bi. Pili Moshi akishiriki kupanda miti katika kisima kirefu cha maji kilichojengwa katika kijij cha Mwagi Mwabilanda.
Kisima Kirefu cha Maji katika kijiji cha Mwagi Mwabilanda.
Mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa akimtwisha ndoo ya maji mmmoja wa akina mama mara baada ya Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzindua mabomba ya maji katika kijiji cha Mwagi Mwabilanda.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa wakifungua mabomba ya maji kuashiria uzinduzi rasmi wa utumiaji wa maji safi na salama ya bomba katika kijiji cha Mwagi Mwabilanda wilayani Kwimba.
Baadhi ya akina mama wakiimba nyimbo wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliowasili katika kijiji cha Mwagi Mwabilanda wilayani Kwimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kata ya Nyambiti tayari kwa kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM ya kata ya Nyambiti, kyutoka kulia ni Mh. Richard Ndasa Mbunge wa jimbo la Sumve, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bi. Pili Moshi na kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ofisi ya CCM kata ya Nyambiti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Nyambiti.
Mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mbele ya Kinana wakati katibu Mkuu huyo alipotembelea kikundi cha wajasiriamali kcha inachojishughulisha na ukamuaji wa mafuta ya Alizeti Lyoma.
Miraji Mtaturu Katibu wa CCM mkoani Mwanza akionyesha kadi za vyama mbalimbali zilizorudishwa kwa CCMna vijana wa kata ya Sumve ambao wamejiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Miraji Mtaturu Katibu wa CCM mkoani Mwanza akionyesha kadi za vyama mbalimbali zilizorudishwa kwa CCMna vijana wa kata ya Sumve ambao wamejiunga na Chama cha Mapinduzi CCM huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Andulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Andulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mkutano katika mji wa Sumve.
Umati wa wananchi ukiwa umejitokeza kwa wingi katika mkutano huo.
Wananchi wakipunga mikono yao kumkaribisha Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano huo.
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza akihutubia mkutano huo.
Wananchi wakipunga mikono juu kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge wa jimbo la Sumve Mh. Richard Ndasa akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Andulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji wa Sumve.
Baadhi ya vijana waliojiunga na Chama cha Mapinduzi leo wakionyesha kadi zao za zamani wakati wakiwa katika chama cha CHADEMA.
Vijana hao wakikabidhi kadi zao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Sumve.
Comments