TIMU YA VITO FC YAAGWA NA KUAHIDI KUREJEA NA USHINDI

1
Balozi wa Finland nchini Tanzania Bibi. Sinikka Antila akifurahia jambo na wachezaji wa Timu ya VITO FC kutoka Kilwa mkoani Lindi, ambayo ilikuwa inaagwa jana kwaa ajili ya kuelekea nchini Finland kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki itakayoanza kutimua vumbi tarehe 05 Julai jijini Helsinki Finland. Timu hiyo imepata ushiriki huo kupitia Asasi ya kirai ya Sports Development Aid (SDA) ikiwa na lengo la kutumia michezo kama nyenzo ya kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto wao wakapate elimu.
2
Meneja Mradi wa Sports Development Aid (SDA) Bw. Mohamed Chigogolo akielezea jambo wakati wa hafla ya kuwaaga watoto wanaoenda kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki nchini Finland, hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Ubalozi wa Finland jijini Dar es Salaam.Katikati ni Afisa Michezo Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bw. Nicholaus Bulamile na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura.
3
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura akipeana mkono wa mmoja wa wachezaji wa timu ya Vito FC ya wilayani Kilwamkoa wa Lindi wakati wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.
4
Balozi wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila akipeana mkono wa mmoja wa wachezaji wa timu ya Vito FC ya wilayani Kilwamkoa wa Lindi wakati wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.
6
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Vito FC ya Kilwa mkoani Lindi wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.
Picha na Frank Shija, WHVUM

Comments