MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI SARAKIKYA APEWA TUZO YA HESHIMA NA TANAPA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MARA 38

????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia  amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake lakini ambapo katika hatua nyingine  atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani  yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa  mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari Mrisho Sarakikya  amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo  ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wamepewa tuzo hizo.
Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Gold Crest.
????????????????????????????????????
Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA akizungumza katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wa pili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wa tatu kutoka kulia, Kutoka kushoto ni Devotha Mdachi Kaimu Mkurugenzi wa (TTB), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Ndugu Baraka Konisaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
????????????????????????????????????
Theophil Makunga Mhariri Tendaji wa Jambo Leo akisoma jina la mmoja wa washindi katika hafla hiyo, Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga na Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga  mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy Sikagonamo mwandishi bora wa  habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa  mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten  Morogoro mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mrimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro  kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti  katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Frank Leonard 
????????????????????????????????????
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA wakiwa katika hafla hiyo kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Pascal Shelutete na  na wa pili ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati akiwa na viongozi wengine katika hafla hiyo kulia ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA , kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga  na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru. 
????????????????????????????????????
Meneja  wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerari Mrisho Sarakikya na mkewe wakitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mwimbaji Mariam akitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akizungumza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Jaji mkuu wa tuzo hizo Dkt. Ayoub Rioba akitambulisha majaji wenzake waliofanya kazi ya kutafuta washindi wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wanenguaji wa bendi ya Utalii  wakitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.

Comments