WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakiwa wamezungukwa na umati mkubwa wa watu wakati alipokwenda kuomba udhamini kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, juzi. Katika tukio hilo maelfu ya wananchi walijitokeza kutaka kumdhamini katika harakati zake za kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais. Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo, lakini aliwataka radhi na kuomba kudhaminiwa na wanachama 45 tu kama matakwa ya CCM yanavyoelekeza.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Singida, Mwamvua Kilo, akizungumza wakati akimkaribisha Nyalandu kuzungumza na maelfu ya wananchi.
Nyalandu akizungumza na wananchi
WANANCHI na wanachama wa CCM wakisikiliza kwa makini wakati Nyalandu akizungumza masuala mbalimbali na kutumia fursa hiyo kuhamasisha umoja na mshikamani ndani ya Chama.
WANANCHI na wanachama wa CCM wakisikiliza kwa makini wakati Nyalandu akizungumza masuala mbalimbali na kutumia fursa hiyo kuhamasisha umoja na mshikamani ndani ya Chama.
WANACHAMA wa CCM wakiimba nyimbo wakati Nyalandu alipokuwa akiingia kwenye viwanja vya Ilongero kuomba udhamini
VIONGOZI wa dini mkoani Singida, wakimpa Nyalandu mkono wa pongezi baada ya kutoa hotuba iliyokonga nyoyo za wananchi wakati alipokamilisha kazi ya kuomba udhamini. Mgombea huyo amepata wadhamini katika mikoa yote nchini.
UMATI ukimsikiliza Nyalandu
Comments