Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA, Edward Greenwood akizungumza wakati wa kuzindua Benki ya FINCA jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya FINCA, Thabiti Ndilahomba akizungumzia kuhusiana na kutoa huduma bora kwa watanzania katika uzinduzi wa benki ya FINCA jijinI Dar es Salaam leo.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA, Edward Greenwood na Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya FINCA, Thabiti Ndilahomba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya FINCA. Picha na Avila Kakingo.
Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya FINCA, Thabiti Ndilahomba akizungumzia kuhusiana na kutoa huduma bora kwa watanzania katika uzinduzi wa benki ya FINCA jijinI Dar es Salaam leo.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
BENKI ya FINCA imewekeza Bilioni 22 ambayo imevuka kiwango cha masharti ya uanzishwaji wa mabenki hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA, Edward Greenwood wakati wa kufunga Taasisi ya mikopo kwa wafanyabiashara wenye kipato cha chini na kuzindua Benki ya Finca katika ofisi za benki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA,Edward Greenwood amesema kuwa watatoa huduma bora kwa watanzania katika maeneo mbalimbali hapa nchini mchini.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 16 na kuendelea kuboresha huduma zao katika benki hiyo.
Greenwood amesema kuwa dhamira yao kubwa katika ufunguzi wa benki hiyo ni kupunguza ugumu wa maisha ya wananchi hapa nchini kwa kutoa kiwango kidogo zaidi kuliko ilivyozoeleka kwa taasisi nyingine za kifedha ili kila mfanyabiashara aweze kufaidika na mikopo katika benki hiyo.
No comments:
Post a Comment