Thursday, February 12, 2026

SERIKALI YAPUNGUZA ADA ZA USAJILI WA VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI; MWANA FA AAGIZA MALIPO YA WAFANYAKAZI YASHUGHULIKIWE NDANI YA WIKI MOJA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji unaoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji unaoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma.








Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji unaoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji unaoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)


Na Mwandishi Wetu

Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa ada za maombi ya leseni kwa vyombo vya habari mtandaoni, kutoka shilingi laki tano hadi 50,000= huku ada ya maombi ikiwa shilingi 10,000/= tu kutoka shilingi 50,000/= hatua inayotajwa kuwa mkombozi kwa wanahabari na wamiliki wa blogu na Online Tv nchini.

Hatua hiyo imetangazwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji unaoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma.

Mbali na kupunguza ada hizo, Mwinjuma ameielekeza TCRA kushirikiana na Bodi ya Ithibati kuhakikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari wanalipwa stahiki zao kwa wakati, wakiwemo wale wanaodai mishahara ya zaidi ya miezi sita.

Amesisitiza kuwa ndani ya wiki moja anatarajia kupokea mrejesho wa hatua zilizochukuliwa kuhusu suala hilo.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwa vyombo vya habari, huku akisisitiza umuhimu wa ubora wa maudhui, kuzingatia maadili ya taaluma na kulinda haki miliki.

“Haki ya kupata taarifa ni ya kila Mtanzania, hivyo vyombo vya habari vinapaswa kuwafikia wananchi wote bila upendeleo,” amesisitiza.

Aidha, amesema Wizara itaendelea kuimarisha mazingira ya sekta hiyo ili wananchi wa vijijini wanufaike na huduma za utangazaji kwa urahisi, sambamba na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo Akili Unde (AI) kwa tija.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Watangazaji Huru Tanzania (NIBA), Amos Ngosha, ameomba Serikali kupunguza wingi wa tozo zinazoikabili sekta hiyo, akieleza kuwa vyombo vya habari hulipa zaidi ya tozo 19 kila mwaka chini ya sheria tofauti, hali inayodhoofisha uwezo wao kifedha na kusababisha baadhi kushindwa kuendelea na huduma au kufungiwa.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Bakari, amesema mwaka 2025 jumla ya wanahabari 2,054 wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo, huku usikivu wa redio ukifikia asilimia 85 na usambazaji wa televisheni kupitia satelaiti kufikia asilimia 100.

Hadi Desemba 2025, jumla ya leseni 770 za utangazaji zilikuwa zimetolewa, huku TCRA ikiwa na mpango wa kuanzisha mfumo wa redio kidijitali ili kuendana na maendeleo ya teknolojia na mahitaji ya soko la mawasiliano.

Mkutano huo wa siku mbili, unaofanyika Februari 12 na 13, 2026, umewakutanisha viongozi na wadau wa sekta ya utangazaji kujadili namna ya kuimarisha na kupanua huduma za utangazaji nchini.

No comments:

Rais Dkt. Samia Awasili Addis Ababa Kushiriki Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi wa AU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Bole, Jij...