Wednesday, March 04, 2015

BAYPORT YAZINDUA TAWI LA KWIMBA MKOANI MWANZA


Na Mwandishi Wetu, Kwimba
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani
Kwimba mkoani Mwanza.
 Meneja Mauzo
wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano
Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel,
katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu.
Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha
na Mpigapicha Wetu.
 
Shughuli za
uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali
wa serikali wilayani humo.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria
kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services,
wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya
Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.
 
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema
kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia
ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa
mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.
 
Alisema
kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za
mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni jukumu lao kutumia
fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha yao.
 
“Serikali
tunaipongeza Bayport Financial Services kwa hatua ya kuanzisha tawi hapa
Kwimba, hivyo tunaamini kwa pamoja tutafanikisha maendeleo kwa watu wote kwa
kupitia njia ya mikopo kwa watumishi wa umma na wafanyakazi waliodhinishwa,”
alisema Emmanuel.
 
Naye Meneja
Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema
kwamba tawi lao limejipanga kutoa huduma bora kwa wakazi na wananchi wa Kwimba
waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma zao

No comments: