Tuesday, June 07, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS WA SAHARAWI, AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA UBELGIJI, BALOZI WA MAREKANI NA KUAGANA NA BALOZI WA ITALY

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa pole kwa Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya kidemokrasia ya Saharawi nchini Mhe. Brahim Buseif alipokwenda ubalozini hapo kutoa pole na kusaini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Rais wa Saharawi Mhe. Mohamed Abdelaziz Mikocheni jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam .PICHA NA IKULU.

No comments:

TANZANIA INA FURSA KUBWA YA KUENDELEZA NISHATI YA JOTOARDHI; WAZIRI NDEJEMBI ALIELEZA BARAZA LA IRENA

📌Asisitiza ushirikiano wa taasisi za kifedha na Jumuiya za Kimataifa hasa katika hatua za utafiti 📌Akaribisha wawekezaji; Asema Serikali i...