Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wenye ualbino, Ikpowose Ero, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana juu ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa watu wenye ualbino Afrika uliofanyika nchini hivi karibuni, Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN, Alvaro Rodrigers na Mkurugenzi mkazi wa Under the same Sun.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imeaswa kupiga vita dhidi ya ukatili, unyanyapaa pamoja na mauaji Watu Wenye Ualbino ili kuweza kila mtu kuishi kwa amani katika nchi yake.
Katika kupiga vita dhidi ukatili na unyanyapaa ya watu wenye Ualbino ni kuweka mkakati wa kuandaa mashitaka kwa ubora zaidi dhidi ya uhalifu wa Ualbino ,kuandaa kanuni za kusimamia waganga wa jadi pamoja na kuimarisha kampeni maalum na endelevu za ufahamu kwa miaka miwili mfululizo ili kupunguza vifo vitavyotokea mara kwa mara.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam uliohusisha nchi 29 Kanda ya Afrika,Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero, amesema mauaji ya watu wenye Ualbino yanaendelea kutokea Barani Afrika na kufanya jamii hiyo kukosa haki ya kuishi kutokana mauaji dhidi yao.
Amesema kuna matukio mengi dhidi ya watu wenye ualbino lakini yamekuwa hayaripotiwi kwa sababu ya usiri katika masuala ya ushirikiana,ushiriki wa familia na ushiriki wa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha.
Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga amesema serikali inatakiwa kuongeza bajeti yake ili watu wenye Ualbino wapate haki sawa katika masuala ya matibabu.
“Serikali ihakikishe kuwa vifaa vya kuimarisha uwezo wa kuona vinapatikana kwa ajili ya mtu m wenye ualbino anapokuwa darasani na kutoa vizuia jua nafuu kama tiba muhimu ili kuziua saratani ya ngozi, ambayo inaendelea kuondoa maisha ya watu hao”amesema Nyanduga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa The Under Sun (TUS), Vick Mtetema amesema kwa pamoja wataendelea kupambana na unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino.
Amesema polisi wa kimataifa na watu wa Uhamiaji washirikiane kwa pamoja ili kulinda watu wanaopitisha watu wenye Ualbino.
Comments