Friday, June 24, 2016

WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI NAMBA 1/2015/2016, CCP MJINI MOSHI

g1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkabidhi zawadi mhitimu Irene Joji (kushoto) kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo.
g3Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji wakimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) jinsi miili yao ilivyokuwa imara kwa pikipiki kupita juu ya matumbo yao. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba
g4Kikosi cha gwaride la heshima kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto jukwaa kuu) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji, Chuo cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo
g5Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji, kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Post a Comment