Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja kunua saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.
Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga (TTCL), Reinhardt (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.
KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa kutumia M PESA bila tozo yoyote.
Makubaliano hayo yaliyofanyika leo viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga foleni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini.
Alisema mteja ataweza kununua Saruji (Simba Cement) kwa kutumia M PESA na hakutakuwa na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote mnunuaji.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.
Alisema Kiwanda cha Simba Cement daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa ununuaji.
Comments