Tuesday, June 07, 2016

RAIS MAGUFULI AFUTA HATI YA MASHAMBA YA MKONGE YALIYOTELEKEZWA MKOANI TANGA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Lushoto, Tanga kabla ya kuelekea Kijiji cha Kibaranga kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.

Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga kilipo kijiji cha Kibaranga, Adadi Rajabu akizungumza baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwaelezea wanakijiji hao uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefuta hati ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya 5,000 yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori ambayo hayaendelezwi kufuatia malalamiko ya wakazi wa zaidi ya 2,000 wa kijiji cha Kibaranga kuhangaikia maeneo ya kilimo na kusababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.

Akizunguza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara,waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni shamba la tano kufutwa na Mheshimiwa Rais katika mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema Serikali mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu utakaowezesha kuwa kila mwananchi apate shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza wananchi.
Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama Mheshimiwa Adadi Rajab amesema watahakikisha wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.

No comments: