Tuesday, June 14, 2016

BALOZI WA CHINA NCHINI AJITOKEZA KUCHANGIA DAMU MUHIMBILI

CHN1
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani akimkaribisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. LU Youqing  ambaye amefika kwenye hospitali hiyo LEO kwa ajili ya kuchangia damu katika maadhimisho ya siku ya damu duniani.
CHN2Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Makani akisoma taarifa fupi kwa Balozi Dk. LU Youqing  kabla ya kuchangia damu LEO.
CHN3Baadhi ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na wa China wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi, Makani wakati akisoma taarifa fupi kwa balozi huyo.
CHN4Balozi wa China, Dk. LU Youqing nchini Tanzania akizungumza na waandishi wa habari LEO katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Makwaia Makani.
CHN5Baadhi ya Madaktari wakimsikiliza Balozi huyo leo katika hospitali hiyo.
CHN6Mkurugenzi wa Upasuaji,  John Kimaro na  Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi, Praxeda Ogweyo wakifuatilia mkutano huo Leo kwenye hospitali hiyo.
CHN7Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali hiyo. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Makani na Balozi wa China, Dk. LU Youqing. 
CHN8Sista Elizabeth Mweta akimwezesha Balozi wa China, Dk. LU Youqing kuchangia damu leo  kwenye hospitali hiyo.
CHN9Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo  akimkabidhi cheti Balozi Dk. LU Youqing baada ya kuchangia damu LEO.
CHN10Balozi Dk. LU Youqing  akinywa chai baada ya kukamilisha shughuli ya uchangiaji damu leo katika hospili hiyo.
Picha na JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
……………………………………………………………………………………………….
Na Neeema Mwangomo, Dar es salaam
Balozi wa China nchini Dk. LU Youqing  leo amejitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuwa na moyo wa kuchangia damu, lakini pia kuadhimisha siku ya wachangia damu Duniani ambayo huadhimishwa Juni 14 kila mwaka.
Balozi  Youqing  amesema wakati  tukiadhimisha  siku hii muhimu, tunatukumbushwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu  kwa upendo ili kuokoa maisha ya wale wenye uhitaji wa damu.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Youqing  amesisitiza kwamba Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika  shughuli mbalimbali ikiwamo  kuisaidia  sekta ya afya .
Awali akizungumza kabla ya shughuli kuchangia damu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Makwaia Makani  amemshukuru Balozi huyo wa China  kwa kuwa Balozi wa kwanza  wa kigeni  kujitokeza kuchangia damu kwenye hospitali hiyo kwani hatua hiyo imeonyesha ni jinsi gani anaguswa  katika kuokoa maisha ya Watanzania.
“Timu   ya  wataalamu mbalimbali wa afya kutoka China wamekua na ushirikiano mzuri na wa muda mrefu na hospitali hiyo katika kusaidia huduma za afya  na tumekuwa tukifanya nao kazi tangu mwaka 1968,” amesema  Kaimu Mkurugenzi Makani.
Akifafanua  amesema  kimsingi mahitaji ya damu  ni makubwa  kwani Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji  chupa za damu  100 hadi 150 kwa siku,  lakini chupa zinazopatikana ni 60 na kwamba upungufu ni asilimia 25.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maabara  wa MNH Dk, Alex Magesa amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Hospitali hiyo  za kukusanya damu, lakini zoezi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo  uchache wa vitanda vinavyotumika wakati wa kutoa damu, jokofu kubwa la kiibailojia kwa ajili ya kuhifadhia damu na usafiri wa kwenda kukusanya damu nje ya Hospitali.
Katika kuadhimisha siku ya wachangia damu duniani  Hospitali ya Taifa Muhimbili inatembelea maeneo mbalimbali  ya wazi  ikiwamo vyuoni  ili kukusanya damu.
Maadhimisho hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma yamebeba  kauli mbiu  ‘Damu inaunganisha kila mtu.’

No comments: