Friday, June 17, 2016

MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA BUNGE LA BAJETI LEO TAREHE 17 JUNI, 2016 MJINI DODOMA

bug1 
Mbunge wa Nchemba (CCM), Mhe. Juma Nkamia akifurahia jambo na Mbunge wa Kaliua (CUF), Mhe. Magnalena Sakaya wakati wakiingia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma  kuanza kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo.
bug2 
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
bug3 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali ya Wabunge leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
bug4 
Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Mhe. Almas Maige akiuliza swali Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
bug5 
Wabunge wa CCM Viti (Maalum) kutoka kushoto, Christine Ishengoma, Martha Umbulla na Magreth Sitta wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo leo.
bug6 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Halima Bulembo, akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo. Kulia ni Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni.
bug7 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akibadilishana mawazo na Wabunge mara baada ya kuahirisha   kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
bug8 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifurahia jambo na Mbunge wa Kibiti, Mhe. Ally Ungando mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO).
Post a Comment