Monday, June 27, 2016

SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA UTAFITI WA KISAYANSI KWENYE SEKTA YA AFYA.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha Muhas pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam mwishoni 
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akizungumza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam .
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa ufungwaji wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam .
 Baadhi ya washiriki wa wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesisitiza utafiti wa kisayansi kwa maendeleo ya taifa na kuhamasisha ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi katika eneo hilo , ili kujenga taifa lenye vijana watafiti na wataalam wa kutosha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  John Michael aliemuwakilisha kwenye ufungaji wa  Mkutano wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema utafiti wa kisayansi ni muhimu kwa nchi yeyote ikiwemo  Tanzania katika  kuhakikisha inafikia  malengo yake ya maendeleo  ya utekelezaji wa wa malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGS).

Aliongeza kuwa utafiti wa kisayansi ni kiungo muhimu katika kuweza kufikia malengo ya SDGS  kwa kuwa ndio unatoa muongozo wa kisayansi na mipango ya namna ya kuyafikia malengo hayo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Ephata Kaaya alisema ni muhimu taifa kuanza kuchukua hatua sasa na kuhakikisha mfumo wa kitaifa wa huduma za afya na uchumi  kwa ujumla  unaweza kukabiliana na mizigo wa magonjwa , kwa njia ya utafiti.

Aidha Prof Kaaya aliwapongeza wanafunzi wa shahada ya uzamili na wahitimu wa MUHAS  waliowasilisha mada takribani  ya 70 kati ya 170  katika mkutano huo na tofauti  na mwaka uliopita ambapo asilimia 30 ya mada ziliwasilishwa na wanafunzi.
Post a Comment