JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA KINGA DHIDI YA MOTO
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idd Chanyika (kulia) akitoa maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa Utawala naFedha, Billy Mwakatage walipotembelea banda hilo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuandikia mmoja ya mwananchi namba ya dharura 114 ambayo hutumika kupokea taarifa ya majanga mbalimbali kutoka kwa jamii.
Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam.
Comments