Wednesday, June 15, 2016

WATENDAJI WABADHIRIFU WA BODI YA MIKOPO KUSHUGHULIKIWA -PROFESA NDALICHAKO

WAZIRI wa Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa  Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana  kuwachukulia hatua watendaji wote waliosimamishwa kati katika wizara ya elimu pamoja na  kuwafikisha vyombo vya dola. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu- Elimu wa Wizara ya Elimu,  Sayansi na Teknolojia, Dk. Leunard Akwilapo.
Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tarish Kibenga Katikati Naibu Katibu Mkuu- Sayansi na Ubunifu, Simon Masanjila na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya  Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Anna Mhere.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa  Joyce Ndalichako ametangaza kiama kwa watendaji wote wa  Bodi ya Mikopo waliofanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu wasiohusika.

Joyce ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.

Amesema kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha vyombo vya dola.

Joyce amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi 2,000 wamepewa mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo vilivyotajwa.

Amesema kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili  ya mikopo ya bodi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati  mikopo kabisa na watoto wa masikini.

Aidha amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za walipa kodi.

Joyce amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya  Elimu na ufundi (NACTE) kufanya kazi kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.

Amesema yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE kufanya kazi kwa uwezo unaostahili

No comments: