Sunday, June 12, 2016

WAFANYAKAZI TBL WAHUDHURIA SEMINA YA MALEZI YA FAMILIA

Watoa mada Grace Makani Tarimo na Dk.Ellivid Waminian wakiongea na washiriki wa semina ya masuala ya kujenga familia bora iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam
m2Wafanyakazi wakisikiliza mada
m4Wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika semina.
……………………………………………………………………………………………………..
Katika kuhakikisha wafanyakazi wake wanapata elimu ya masuala mbalimbali ya kijamii nje ya mazingira ya kazi,kampuni ya TBL Group imewezesha baadhi ya wafanyakazi wake kuhudhuria semina ya malezi  ya familia iliyofanyika jijini Dar es Salaam .
Katika semina hiyo wataalamu mbalimbali  wa masuala ya elimu jamii kutoka kampuni ya Grace Inc walitoa mada kuhusiana na masuala ya malezi bora ya familia na changamoto zilizopo katika kujenga familia bora ambapo washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali yanaohusiana na malezi ya familia.
Wafanyakazi hao walishukuru kampuni kwa kuwapatia fursa ya kuhudhuria semina hiyo na walisema kuwa imewawezesha kupata maarifa mbalimbali yatakayowasaidia kujenga familia zao.
Post a Comment