Tuesday, June 14, 2016

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baadya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao  wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
SIL2Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
SIL3Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli (katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo asubuhi mjini Dodoma.
SIL4Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
SIL5Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishina Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akibadilishana mawazo na Mbunge wa Sengerema (CCM), Mhe. William Ngeleja na Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), Mhe.  Hamoud Jumaa (CCM)  mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.
SIL6Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
SIL7Wabunge wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo .(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)

No comments: