Wednesday, June 29, 2016

PBZ YAADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 50 KWA KUSAIDIA JAMII NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA KIDONGOCHEKUNDU.

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akizungumza na Maofisa wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakati wa kikabidhi msaada wa magodoro kwa ajili ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akimkabidhi msaada wa magodoro 100 Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza akitowa shukrani kwa PBZ  kwa msaada wao huo wa magodoro umeletwa wakati muafaka na kuwata taasisin nyengine kujitokeza kutoa misaada.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg.Juma Ameir akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Kidongochekundu Zanzibar Ndg. Haji Vuai Hilal, wakati walipofika katika hospitali hiyo ya Mental kutowa misaada ya mashuka 200 kwa ajili ya hospitali hiyo. katikatika Afisa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Nuhu. 
Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Haji Vuai Hilal. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir akizungumza na Uongozi wa Hospital ya Mental Kidongochekundu Zanzibar wakati wa kutembelea hospitali hiyo na kutoa msaada wa mashuka 200 ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo.
Post a Comment