Monday, June 13, 2016

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAWAPIGA MSASA MAWAKALA WAKE

b1Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akizungumza na Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzo ya mawakala hao katika kutoa huduma bora kwa wateja na mikakati ya  kuuza bidhaa za shirika hilo kwa ufanisi mafunzo hao yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya watendaji kutoka vitengo kadhaa ambao pia walitoa mada kadhaa katika kuboresha huduma za shirika la Bima.
b2Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akifafanua jambo  kwa Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzohayo yaliyofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Bima la Taifa NIC jijini Dar es salaam.
b3Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini maelezo ya Bi Rose Lutu Kaimu Mkurugenzi wa NIC.
b4
Mafunzo yakiendelea.
b5b6Kaimu Mkurugenzi wa MasokoElisante Maleko akimuelekeza jambo kwenye ratiba Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC  ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo.
b7Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC  ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo akiandika mambo muimu yaliyokuwa yakijadiliwa katika mafunzo hayo.
b8Kaimu Mkurugenzi wa MasokoElisante Maleko kulia akiwa pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Post a Comment