Wednesday, June 08, 2016

MWAKILISHI WA JIMBO LA MALINDI AKABIDHI MSAADA WA SH. MILIONI MOJA NA LAKI TATU KWA AJILI YA UNUNUZI WA VIFAA VYA MAJI

MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Maliasili na Usafirishaji Zanzibar akizungumza na Msaidizi wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour (kulia) kabla ya kumkabidhi Msaada huo.
MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akimkabidhi fedha taslimu (sh.1,300,000) Msaidizi wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya bomba la maji lilopasuka Mtaa Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini Zanzibar.
MSAIDIZI wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour akimshukuru Mwakilishi wa Jimbo hilo mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.
MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akijionea maji sehemu inayovujisha Hapo Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini Zanzibar.(picha na Abdalla Omar - Habari Maelezo Zanzibar.
Post a Comment