Sunday, May 08, 2016

RAIS MSTAAFU AWAMU YA NNE DKT JAKAYA KIKWETE AMUWAKILISHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA


Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa ajili ya maziko hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta.
Naibu Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio hilo.
Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta,Bi Margaret Kenyatta. 
Rais Mstaafu wa Kenya,Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.

Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

No comments: