Monday, May 23, 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU AG NA MSHAURI WAKE WA UCHUMI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.
  
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Mei, 2016

No comments: