HOSPITALI YA MUHIMBILI YAFUNGA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA MATATIZO YA MOYO JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.
Katibu mkuu na mkurugenzi wa Muntada Aid, Sheikh Khalid Sukeir akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Balozi wa Qatar, Wajih Al Uteibly akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia na Qutar na baaadhi ya madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka nchi za Saudi Arabia na Qutar jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja taasisi nne kutoka nchi tatu tofauti.
Abri amesema taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya hapa nchini na Taasisi ya Jakaya Kikwete.
Amesema kuwa kambi hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.
Kwaupande wake Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao wametibiwa hapahapa nchini.
Comments