Bonanza maalum kwa ajili ya wanavyuo wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki (Mei 21, 2016) Jijini Arusha lilifana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakijiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
Viongozi wa vyuo mbalimbali mkoani wakiwa katika picha ya pamoja Afisa Mfawidhi wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina (wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma) baada kikao cha maandalii kilicho fanyika katika ofisi za PSPF mkoa wa Arusha.
Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini Arusha, lilijumuisha vyuo vya Makumira, Mt. Meru, SAUT, MAN U (Chuo Kikuu cha Arusha), Chuo cha Ufundi Arusha na IAA.
Wanachuo wa IAA, wakishangilia baada ya timu yao kuibuka mshindi katika mpira wa miguu.
Michezo iliyoshindaniwa ni pamoja na Football, Netball, Basketball na Volleyball, hata hivyo mchezo uliovuta hisia za washiriki wengi ni mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya Chuo cha Uhasibu Arusha kilibuka mshindi
Wanachuo wakifatilia Burudani kutoka kwa Mjomba Band
Akifungua mashindano hayo, Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Bw. Daniel Machunda aliwataka wanavyuo hao kutumia michezo hiyo kama sehemu ya kujenga uhusiano Mwema na ushirikianao kati ya vyuo na kati ya yao wenyewe.
Pia aliishukuru PSPF kwa kuandaa Bonanza hilo ambalo msingi wake mkubwa ulikuwa ni kuwaelimisha wanavyuo juu ya huduma za PSPF. “Hili jambo mnalofanya PSPF ni jambo zuri sana kwa wanafunzi wa vyuo vya Arusha pamoja kutoa burudani lakini pia mnawapatia ufahamu juu ya Mfuko wenu (PSPF), hili ni jambo zuri sana na ninawaomba wana vyuo kuazingatia elimu mtakayopatiwa na wakati ukifika mfanye maamuzi sahihi,” alisema Bw. Machunda.
Ukaguzi wa timu kabla ya mchezo, wa tatu kulia ni Afisa Mfawidhi wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina.
Kwa upande wake Afisa mchezo wa Mkoa wa Arusha, alisema amefurahishwa sana kwa PSPF kuandaa Bonanza hilo kwa wanavyuo wa mkoa wa Arusha na kuwataka wanavyuo kuhakikisha mashindano yanaanza na kumalizika kwa usalama, lengo likiwa ni kudumisha upendo na uhusiano Mwema kati ya vyuo hivyo.
Wawakilishi wa vyuo vilivyoibuka washindi katika bonanza hilo wakiwa na katika picha pamoja na Mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa mkuu wa Chuo cha Uhuasibu Arusha, Bibi. Laura Kishala Aliishukuru PSPF kwa kuweza kuanda Bonaza hilo kwa vyuo vya Arusha, akifafanua zaidi alisema, “Bonanza hili mliloliandaa hakika ni jambo zuri sana kwa wanafunzi wetu kwani michezo ni afya, na pia tunashukuru kwa elimu juu ya Mfuko wa PSPF, nina imani sasa wanafunzi wetu wamepata elimu ya kutosha juu ya PSPF, “.
Pamoja na mashindano hayo, pia wanavyuo hao walipata burudani kutoka kwa balozi wa PSPF Mrisho Mpoto, ambaye alikuwa na kikundi chake cha sanaa. Mpoto alikuwa ni burudani tosha kwa wanavyuo hao.
Baada ya kupata elimu juu ya Mfuko, hususan katika Mpangowa uchangiaji wa hiari (PSS), idadi kubwa ya wanavyuo hao walijiunga na mpango huo.
Wanavyuo wakijiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS)
Wanavyuo wakijiunga na Mpango wa Uchagiaji wa Hiari(PSS)
“Hawa jamaa (PSPF) wapo vizuri sana, kwani wametupatia burdani na elimu ya kutosha juu ya PSPF, hakika sasa nimepata uelewa wa kutosha juu yao na ukifika wakati wa kuchagua Mfuko nitafanya maamuzi sahihi,” alisikika mmoja wa wanavyuo hao.
Comments